MWANA FA: SERIKALI ITALETA MAKOCHA WA NGUMI KUTOKA CUBA


 ********

Naibu waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo mhe. Hamis Mwinjuma amesema serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia baraza la taifa la michezo litaleta wakufunzi wa mchezo wa ngumi nchini.

 Naibu waziri Hamis Mwinjuma amesema hayo wakati wa kikao na waandaaji wa mapambano ya ngumi kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa manispaa ya Temeke ambapo ametoa maelekezo kwa baraza la michezo la taifa kusimamia utekelezaji wa mchakato huo.

 "Niwaelekeze baraza la michezo kuwatafuta wakufunzi kutoka Cuba ambao mtawalipa na kuwalipia gharama zao waje hapa tukusanye makocha wetu wanaofundisha ngumi wapitie semina, clinis na kozi ndogondogo lakini kila kocha ambaye anafundisha mtu atakayekuja kupanda ulingoni kupigana ni lazima awe amepita humo.

"Haya sisi tutasimamia ili kuhakikisha kila mtu ana fursa sawa ya kufanya kama kutakua na ada itakua ni ndogo sana lakini serikali itabeba mzigo huu kuhakikisha walimu wetu wanapitia kwa wakufunzi na wanapata ushahidi kwa maana ya vyeti kuhakikisha wanafundisha kwa usahihi mabondia wanakuja kupanda kwenye ulingo ambazo sisi tunaangalia kama mchezo. 

"Kamisheni hili la kwenu na baraza litasimamia kuleta hawa wakufunzi na kamisheni  mtahakikisha walimu wetu wote wanaofundisha ngumi mabondia wanaokuja kupanda ulingoni wanapitia kwenye semina hizi,"amesema naibu waziri huyo.

@tpbrctz_official

@wizara_sanaatz

0/Post a Comment/Comments