MWANDISHI WA AYO TV ATOWEKA SIKU TISA

*****

Mwandishi wa Habari Eugen Peter anatafutwa na Familia yake pamoja na Ofisi yake ya @AyoTV_ Dar es salaam baada ya kutoweka bila kujulikana alipo leo ikiwa ni siku ya tisa.

Mara ya mwisho Eugene alionekana mazingira ya nyumbani kwake Jumapili December 29,2024 majira ya saa mbili usiku.

Familia akiwemo Baba yake Mzazi na Watu wa karibu wamethibitisha kutokuwa na mawasiliano naye tangu wakati huo ambapo Dar es saalam hajaonekana na kwao Arusha na Moshi hajafika huku simu zake zikiwa hazipatikani.

Baada ya jitihada kubwa za kumtafuta maeneo mbalimbali na kutoa taarifa ya kupotea kwake Polisi, AyoTV na Familia kwa pamoja wameomba Mtu mwenye taarifa kumuhusu apige simu namba 0769401050 au aripoti kituo cha Polisi kilicho karibu nae

ccMillardayo

 

0/Post a Comment/Comments