PROF. KITILA MKUMBO AWAPIGA MKWARA WANAOTUMIA JINA LAKE KUSAKA UBUNGE

*********
Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amewataka Wananchi wa Jimbo la Ubungo lililopo Jijini Dar es Salaam kuwa makini na watu wanaosaka Ubunge wa Jimbo hilo kwa kutumia jina lake.

Prof. Kitila amesema Mwaka huu 2025 atachukua Fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo na amejipanga kupambana na Hali yoyote atakayokutana naye kwenye mapambano maana Uchaguzi ni mapambano na Yeye ni mzoefu wa masuala ya Siasa.

Kuhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk. Samia Suluhu Hassan Prof. Kitila amewakumbusha Wana Ubungo kuwa kwa tamaduni na taratibu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais anapaswa kusalia madarakani kwa mihula 2 na kuwataka wanaCCM kuelekeza Kura zao kwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan.














0/Post a Comment/Comments