RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

****

Rais wa Tanzania .Dkt.Samia Suluhu Hassan, amemteua Jaji Mstaafu Beatrice Rhoda Mutungi, kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Rufani za Kodi (TRAT), Jaji Mstaafu Mutungi anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Gad John Mjemmas ambaye amemaliza muda wake

Rais Samia amemteua Dkt. Diwani Bakari Msemo, amemteua Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dkt. Msemo ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, anachukua nafasi ya Dkt. Julius David Mwaiselage ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Pia Rais Samia amemteua CPA. David Carol Nchimbi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NMB Plc. CPA, Nchimbi anachukua nafasi ya Dkt. Edwin Mhede ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.


 

0/Post a Comment/Comments