*******
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC- Organ), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Mkutano wa Dharura wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi hiyo unaofanyika kwa njia ya mtandao katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 5 January, 2025.
Viongozi wengine walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja
na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi
Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt.
Stergomena Tax ( Mb.), Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi, Dkt. Samwel Shelukindo pamoja na Katibu Mkuu Wizara
ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe.
Post a Comment