****
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema hajawahi kusema mtu asilipe kodi, ( maelekezo kutoka juu ) na ikitokea haja ya kufanya hivyo, shirika au mtu asilipe kodi, nitafanya kwa maandishi na sio mtu aje kwa mdomo
“Mimi sijawahi kutoa maelekezo mtu asilipe kodi, na ikitokea haja ya kufanya hivyo, shirika au mtu asilipe kodi, nitafanya kwa maandishi na sio mtu aje kwa mdomo, maelekezo kutoka juu, mimi sijawahi kufanya hivyo,” amesema Rais Samia huku akisisitiza umuhimu wa kulipa kodi.
Rais Samia ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 23, 2025 akizungumza katika hafla ya utaoaji tuzo kwa walipa kodi bora wa mwaka 2023/2024 ya TRA inayofanyikia katika Ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam.

Post a Comment