SIMBA inayonolewa na Kocha
Mkuu, Fadlu Davids imeweka wazi kuwa inakwenda kukutana na mpinzani mgumu ndani
ya dakika 90 kutokana na mwendo wake wa kupata matokeo mazuri kwenye mechi za
nyumbani ndani ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Wakiwa na kumbukumbu ya kupata
matokeo chanya kwenye mchezo waliocheza nao Bravos, Uwanja wa Mkapa Novemba 24
2024 ubao uliposoma Simba 1-0 Bravos, watakabiliana nao kwa mara nyingine,
wakiwa ugenini.
Tayari kikosi cha Simba
kimewasili Angola kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo unaotarajiwa
kuchezwa Januari 12 2025 kwa wababe hao kutoka kundi A kusaka pointi tatu
muhimu katika kusaka tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali huku kocha akisema
kuwa ni mchezo mgumu kwao.
“Tunakwenda kucheza mchezo
mgumu hasa ukizingatia kwamba wapinzani wetu Bravos wamekuwa na mwendo mzuri
kwenye mechi ambazo wanacheza wakiwa nyumbani hivyo tunakwenda kwa tahadhari na
malengo ni kuona kwamba tunapata ushindi.
Post a Comment