SOUTH AFRICAN AIRWAYS YATUA DAR RASMI


******

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA) Salimu Ramadhani Msangi amesema kurejea kwa  safari za Shirika la Ndege la Afrika Kusini kutakuza uchumi wa nchi kwa kuongeza mapato ya wageni wanaoingia na kutoka nchini.

Hayo ameyasema leo Mkurugenzi huyo Usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salaam kwenye uzinduzi wa Safari za  Shirika la Ndege la Afrika Kusini (South African Airways) nchini  ambapo kipindi cha nyuma huduma hizo zilisimama kutokana na sababu mbalimbali.

Msangi amesema hatua hiyo ina tija kwa nchi kwani wanaongeza Shirika lingine la ndege ambapo itaongeza idadi ya abiria wanatumia Kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere.

Aidha Msangi amesema safari hizo zitaongeza ajira kwa watanzania  ikiwemo kuhudumia hiyo ndege hivyo mashirika mengine yanaona kuna fursa ya kuja kuwekeza nchini.

"Ukiangalia kihistoria Tanzania na Afrika ya Kusini tumekuwa na mashirikiano ya karibu sana kibiashara  kwa hiyo watanzania wengi walikuwa wanahitaji ndege inayokwenda Afrika ya Kusini wakafanye Shughulo zao  watu wa Afrika Kusini pia walikuwa  wanahitaji ndege ambayo inakuja  Tanzania ili wafanye biashara zao.

"Tulikuwa na Ndege ndogo bado ipo lakini uwezo wake sio kama ndege ilikuja leo  kwa hiyo tunapopata ndege kubwa kama hii tunaongeza idadi ya Abiria ambao wanakwenda katika nchi hizi mbili sisi hii ni hatua kubwa kwa kiwanja hiki tunazidi kuongeza mapato pia tunaleta ajaira na inasaidia ndege nyingine kuona kiwanja hichi kina huduma bora" amesema Msangi

Aidha kuhusu usalama wa  wa anga Msangi amesema   kwa sasa hivi usafiri wa anga umeimarika  hivyo hawana matukio yeyote makubwa ya kiusalama kwenye anga wala matishio yeyote yanayoathiri usafiri wa anga .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)Abdul Mombokaleo amesema kurejea kwa safari hizo za ndege kutakuwa na tina kwa Taifa huku akisema kiwanja cha Mwalimu Julius Nyerere ni bora duniani kwa sababu inafata miongozo duniani kwa mujibu wa mamlaka za anga  za dunia.

" Ujio wa ndege hizo unaongeza chachu kwanza ushindani kwa maaana kwamba hata shirika letu la nyumbani tunaipa nafasi ya kushindana kwa sababu pia nao wanaenda Afrika Kusini  lakini pia tunaongeza wigo wa abiria wataokwenda na kurudi Afrika kusinukwa maana kwamba waafrika kusini watawenza kuja Tanzania na watanzania wataenda Afrika Kusini hii inachachua na kuongeza  kasi ya ukuaji wa uchumi" amesema Mombokaleo .

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la ndege la Afrika Kusini (South African Airways )Prof. John Lamola amesema sekta ya anga ni muhimu baina ya nchi zote mbili hivyo mashiriano hayo ya mda mda mrefu ya hivyo ni muhimu kuungana ukiachana na sababu ya ugonjwa wa Covid 19 kusitisha safari hizo hivyo umoja na mshikamano ni mzizi uliosababisha  kurudi kw safari hizo nchini itakuza kukuza sekta hiyo ya usafiri baina ya pande mbili.





0/Post a Comment/Comments