TANESCO, TOENI TAARIFA ZA KUKATIKA KWA UMEME ILI WANANCHI WAJIPANGE


 ******

Na Mwandishi Wetu 

Hivi karibuni kukatika kwa umeme ghafla kumeanza kuwa jambo la kawaida, jambo linalosababisha changamoto kubwa kwa wananchi hasa katika shughuli zao za kiuchumi. 

Mara nyingi, umeme unapokatika, hakufuatwi na taarifa yoyote kutoka kwa Mamlaka husika yaani Shirika la Umeme Nchini, TANESCO, kuhusu sababu au muda wa kurejea.

 Hii imekuwa kero kubwa, kwani wananchi wanakosa fursa ya kupanga ratiba zao kwa kuzingatia masuala ya umeme. 

Nilijaribu kupitia kurasa rasmi za TANESCO kwenye mitandao ya kijamii,baadhi ya vyombo vya Habari lakini nilikosa taarifa yoyote kuhusu mgao wa umeme au matatizo yaliyosababisha kukatika kwa umeme. 

Hii inaonyesha udhaifu katika mawasiliano ya shirika hilo na wananchi.

Wananchi wanahitaji taarifa sahihi na kwa wakati ili waweze kujipanga na kuepuka usumbufu. 

Ikiwa ni mgao, basi TANESCO wanapaswa kutangaza na kutoa ratiba ili watu waweze kupanga shughuli zao kiuchumi bila usumbufu. 

Pia, maoni ya watu katika mitandao ya kijamii yanaonyesha kuwa wengi wanakumbwa na changamoto hii ya kukatika kwa umeme bila taarifa yoyote rasmi Hivyo, ni muhimu kwa TANESCO kutatua tatizo hili la mawasiliano na kuhakikisha wananchi wanapata taarifa zinazohitajika ili waweze kukabiliana na hali hii kwa ufanisi.






Hayo ni baadhi ya maoni ya watu juu ya kero ya kukatika kwa umeme katika siku za hivi karibuni yalituma katika ukurasa wa Tanesco wa mtandao wa kijamii

0/Post a Comment/Comments