TANZANIA YAPANGA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA NISHATI YA UMEME BORA


.............

NA MUSSA KHALID 


Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), na Umoja wa Afrika, inalenga kuimarisha upatikanaji wa nishati ya umeme bora, nafuu, na endelevu kufikia waafrika milioni 300 kufikia mwaka 2030. 

Hayo yameelezwa Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa serikali Gerson Msigwa wakati akifungua warsha maalum ya wahariri Mwandishi wa habari wa kuelekea mkutano wa wakukuu wa nchi za Afrika kuhusu nishati unaotarajiwa Kufanyika January 27 na 28 mwaka huu.

Msigwa amesema Tanzania inajivunia kuwa mwenyeji wa mkutano huo mkubwa kwani unalenga kuharakisha ukuaji wa mageuzi katika nishati barani Afrika. 

Aidha amesema Katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2024, Serikali imefanikiwa kufikisha umeme katika vijiji 12,278, sawa na asilimia 99.7 ya vijiji vyote.

Awali akizungumza Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Innocent Luoga amesema kuwa Katika Bara la Afrika takriban watu milioni 685 bado hawajafikishiwa huduma ya umeme kati ya watu zaidi ya Bilioni 1 , hivyo Benki ya Dunia (WB) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) hivi karibuni walitangaza ushirikiano wa kihistoria utakaosaidia kuharakisha ufikishaji wa umeme kwa watu milioni 300 barani Afrika ifikapo 2030.

0/Post a Comment/Comments