Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa
ya uwepo wa kimbunga “DIKELEDI” katika Bahari ya Hindi mwambao wa pwani ya
Msumbiji.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Mamlaka
hiyo leo imeeleza kuwa Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa kimbunga hicho kwa
sasa kipo katika mwambao wa pwani ya Msumbiji na kinatarajiwa kurejea katika
Rasi ya Msumbiji leo Alasiri.
Imesema kwa sasa, kimbunga hicho hakiashirii uwezekano wa kusababisha athari za moja kwa moja hapa nchini ambapo kutokana na ukaribu wa maeneo ambayo kimbunga “DIKELEDI” kipo sambamba na maeneo ya kusini mwa nchi upo uwezekano mdogo wa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa katika maeneo ya Pwani ya kusini hususan katika Mikoa ya Lindi na Mtwara kwa siku ya leo tarehe 14 ya Januari, 2025.
Post a Comment