******
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi Utabiri wa Msimu wa Mvua za
Masika 2025 kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka.
Akizungumza na waandishi wa
Habari mapema leo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA,
Mwakilishi wa Kudumu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Makamu
Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na
Tabianchi, Dkt. Ladislaus Changa amesema mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani
zinatarajiwa katika maeneo mengi ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki pamoja na
Mashariki mwa mikoa ya Mara na Simiyu huku mvua za Wastani hadi Chini ya
Wastani zikitarajiwa katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini, Kaskazini mwa Mkoa wa
Kigoma na Ukanda wa Ziwa Victoria.
“Mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya Nyanda
za Juu Kaskazini Mashariki pamoja na Mashariki mwa Mikoa ya Mara na Simiyu.
Aidha, mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo ya
Pwani ya Kaskazini, Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma na Ukanda wa Ziwa Victoria
(Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga na magharibi mwa mikoa ya Simiyu na
Mara) katika kipindi cha Msimu wa Masika, 2025.” Amesema Dkt. Chang’a
Vilevile, taarifa hiyo imeelezea pia ongezeko la mvua linatarajiwa katika
kipindi cha mwezi Aprili sambamba na kutoa angalizo la matukio ya hali mbaya ya
hewa ikiwemo vipindi vya mvua kubwa kujitokeza hata katika maeneo
yanayotarajiwa kupata mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani.
Akizungumzia athari zinazoweza kujitokeza, Dkt. Chang’a amesema Mvua za Wastani
hadi Chini ya Wastani zinazotarajiwa katika baadhi ya maeneo zinaweza kupelekea
upungufu

Post a Comment