TMDA YAPAA VIWANGO VYA JUU USIMAMIZI WA DAWA AFRIKA


 *****
Na Tausi Mbowe 

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), imejipatia umaarufu mkubwa katika umakini wa mifumo yake ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba katkka nchini nyingine duniani ikiwamo bara la Afrka. 

Hivi karibuni, Mamlaka ya Usimamizi wa Dawa nchini Boswana 

(BoMRA) na maafisa kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika- Mpango wa Maendeleo ya Afrika (AUDA-NEPAD) walifanya ziara tofauti katika TMDA ili kujifunza mfumo wake bora na udhibiti na  ufanisi katika udhibiti. 

Katika ziara hiyo iliyofanywa Januari, 2025 wajumbe wa bodi  ya MoMRA walipatiwa uzoefu wa shughuli za Mamlaka hiyo  ya Dawa nchini Tanzania. 

Ujumbe huo ulitembelea ofisi za TMDA zilizopo makamu makuu ya nchini jijini Dodoma na mkoani Dar es Salaaam. 

Katika ziara hiyo wajumbe hao waliona michakato ya tathimini, uchambuzi usajili pamoja na ukaguzi wa bidhaa. 

Sambamba na hilo, ujumbe huo ulijulishwa kuhusu mfumo wa ufuatiliaji na madhara yatokanayo na matumizi ya dawa na vifaa tiba. 

Pia, taatibu bora za huduma kwa wateja na miundombinu ya kisasa ya kielekroniki. 

Ujumbe huo uliahidi kutekeleza mbinu bora za TMDA katika kubkresha udhibiti nchini kwao wakitambua uwezekano wa kuboresha viwango vya udhibiti nchini Boswana.

Aidha, katika tathimini iliyofanywa na AUDA- NEPAD mwishoni mwa Februari 2024 uwezo wa TMDA kuongoza mradi wa ufuatiliaji wa athari za dawa kwa bara la Afrika unaojulikana kama 'AU35' ulipimwa kwa undani na kuleta matokeo chanya. 

Safari ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), kuelekea ubora ilianza nwaka 2003 baada ya kubadilika kutoka Bodi ya Phamarcy hadi kuwa mfano wa taasisi ya ufanisi katika udhibiti.

0/Post a Comment/Comments