Shirika la Reli Tanzania (TRC), limewapa pole abiria waliokuwa wakisafiri kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma January 8, 2025 kufuatia usumbufu uliojitokeza kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyotokea katika kituo cha lhumwa Dodoma majira ya saa 5:38 usiku.
TRC imesema inajua safari za kawaida kati ya Dar es salaam na Dodoma zimeathirika na hilo inaweza kuwa na athari kubwa kwa abiria.
Taarifa iliyotolewa na TRC usiku huu imesema “Mafundi wetu wamepambana kurekebisha tatizo husika na kuhakikisha huduma zetu zinarejea kwenye hali ya kawaida’’
Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa “treni zilizoathirika ni treni iliyoondoka saa 12.55 jioni siku ya Jumanne January 7, 2025 kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma iliyotarajiwa kufika 5.01 usiku badala yake ilifika saa 7 usiku, treni inayoondoka saa 11.15 asubuhi siku ya Jumatano January 8, 2025 kutoka Dodoma kuelekea Dar es salaam iliondoka saa 3.05 asubuhi, treni iliyotakiwa kuondoka saa 12.00 asubuhi January 8, 2025 kutoka Dar es Salaam kueleka Dodoma iliondoka saa 12.30 asubuhi na treni iliyotakiwa kuondoka saa 3.30 asubuhi siku ya Jumatano January 8, 2025 imeondoka saa 11.55 kutoka Dar es Salaam Kuelekea Dodoma”
Post a Comment