******Tanzania
itaendelea kutoa ushirikiano kwa Ubalozi wa Marekani nchini na kuahidi kumpatia
ushirikiano wa karibu Balozi ajaye katika utekelezaji wa majukumu yake awapo
Tanzania pamoja na kuangazia maeneo ya kuongeza wigo wa ushirikiano kwa manufaa
ya nchi zote mbili.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Mahmoud Thabit Kombo, akimuaga Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Michael
Battle anayetarajiwa kuondoka nchini hivi karibuni.
Waziri
Kombo amemshukuru Balozi Battle kwa ushirikiano mzuri kati ya wizara na ubalozi
katika kipindi chote cha uongozi wake pamoja na kufanya kazi kwa karibu na sekta na wizara mbalimbali za kimaendeleo
nchini.
Aidha,
ametumia fursa hii kutoa salamu za pole kwa msiba wa Rais Mstaafu wa Marekani,
Hayati Jimmy Carter aliyefariki Dunia Desemba 29, 2024.
Kwa upande
wake, Balozi Battle amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake katika kuleta maendeleo Tanzania
lakini pia kwa utayari wake katika shughuli za ushirikiano.
Ameomba pia Wizara kumpa ushirikiano wa karibu Kaimu Balozi atayekuwepo wakati Marekani ikingoja kutuma Balozi mwingine.
Post a Comment