WAZIRI SILAA ALITAKA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA –TPC, KUONGEZA UBUNIFU.


...........................

NA ISSA MOHAMMED

Waziri wa Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari Jerry Silaa amelitaka Shirika La Posta Tanzania liongeze kasi, ubunifu kwenye teknolojia ya mawasiliano ili liweze kuleta tija na ufanisi kwenye Shirika hilo pamoja na nchi.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam kwenye Uzinduzi wa baraza kuu la wafanyakazi wa Shirika la Poata na mkutano wa 31 wa baraza kuu la wafanyakazi hao.

Silaa ameelekeza Shirika hilo kila mtumishi akafanye kazi kwa weledi uzalendo na ubunifu, wangalie maswala yote yaliyotolewa ahadi bungeni wakati wa uwasilishaji wa bunge la bajeti mwaka wa fedha 2023/24,kuendelea kufatia majukumu mbalimbali na kufuata sheria mpya ya manunuzi.

Aidha Silaa amesema Shirika liwe bunifu katika utoaji huduma,Shirika lihakikishe linafanyia kazi hoja zote za ukaguzi,mikakati wanayopendelea isiwe ya kufikirika iwe yenye uhalisia na inayotoa matokeo tarajiwa, wataalam wa ndani wahakikishe wanatekeleza majukumu nyeti ya shirika na mafunzo kwa watumishi yatolewe mara kwa mara ili kuongeza tija.

"Ndugu wajumbe serikali kwa upande wake itaendelea kuweka sera , sheria , kanuni, stahiki pamoja na kujenga na kuboresha miundombinu ya kitaifa kama vile mkongo wa mawasiliano , anuani za makazi, kuimarisha njia za usafirishaji na mawasiliano ili kurahisisha utoaji wa huduma za Posta na usafirishaji wa haraka.

"Tutaendelea kushughukia changamoto zinazoleta mkwamo katika maendeleo kama vile malimbikizo ya madeni ya kodi dhamira ikiwa ni kuwa na mazingira wezeshi na rafiki katika utekelezaji wa majukumu yenu "amesema Silaa

Kwa upande wake PostaMasta Mkuu Macrice Daniel Mbodo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo amesema katika kuhakikisha yanakuwepo mahusiano mazuri katika taasisi hiyo baraza la wafanyakazi lina dhumuni la ushirikishwaji wa watumishi katika maamuzi yanayohusu utekelezaji wa mipango na bajeti iliyopita na mipango ijayo.

" Kwa Shirika letu la Posta Tanzania baraza hili la wafanyakazi ni baraza la kumi tangu kuanzishwa kwa shirika na baraza hili lina jumla ya wajumbe 87 mkutano wa 31 wa baraza kuu la wafanyakazi unatarajiwa kuwa na mambo makuu mawili ambayo ni mafunzo kwa wajumbe wa baraza pamoja na kikao chenyewe cha baraza"amesema Macrice.

0/Post a Comment/Comments