******
Takwimu zimeonesha kuwa kiwango cha upatikanaji wa huduma za kifedha Nchini Tanzania umeongeza hadi kufikia asilimia 89 kutoka asilimia 79 mwaka 2023 huku elimu ya fedha pamoja na urahisi wa upatikanaji wa huduma hiyo hasa maeneo ya Vijijini imetajwa kuchangia ukuaji huo.
Katika kuendeleza huduma hizo za kifedha Nchini, Benki ya Azania imezindua mfumo mpya wa huduma za kibenki Kidijitali uliopewa jina la ‘’Azania Digital’’ utakaojielekeza katika kutoa suluhisho la kibenki kwa wateja wake kote Nchini.
Akizungumza Jijini Dar es salaam katika uzinduzi huo, Mkuu wa idara za benki kidijitali benki ya Azania, Vinesh Davda amesema mfumo huo utajikita katika kutoa huduma mbalimbali za kibenki ikiwemo kwa njia ya WhatsApp, Wakala pamoja na njia ya simu.
Kwa upande wake Meneja mwandamizi huduma za wateja binafsi wa benki hiyo Jackson Lohay amesema Benki ya Azania imeongeza Mawakala katika maeneo mbalimbali ili kufikisha huduma za kibenki na kuongeza ujumuishi wa kifedha.
Aidha kiwango cha watu walio nje ya huduma rasmi za kifedha bado umeendelea kuyakumba baadhi ya makundi ikiwemo wakulima wadogo, Vijana na Wanawake ambapo uzinduzi wa Azania Digital utasaidia kuongeza ubunifu kwenye sekta hiyo.
Post a Comment