BONDIA WA TANZANI JAMAL KUNOGA KUPANDA ULINGONI NCHINI KAZAKHSTAN

**** 

Bondia Jamal Kunoga kutoka Tanzania anatarajia kupanda ulingoni kwaajili ya pambano lake dhidi ya mpinzani wake Samat Zhetibayev wa nchini Kazakhstan.

Kunoga anatarajiwa kupigana na Zhetibayev kwenye pambano litakalofanyika Februari 23, 2025 katika ukumbi wa Halyk arena sport complex uliopo Aktau nchini Kazakhstan.

Kunoga atacheza na mpinzani wake huyo katika pambano hilo lisilo la ubingwa la uzani wa 'bantam' ambapo litakua la raundi sita.

Mara ya mwisho Kunoga kupanda ulingoni ilikua Oktoba 25, 2024 ambapo alimtandika bondia Elly Ally kwa 'points' za majaji wote watatu katika ukumbi wa Tanzanite uliopo mkoani Morogoro.

Kunoga ni bondia namba saba nchini Tanzania katika mabondia 51 pia ni wa 209 kati ya 1149 Duniani huku akiwa na hadhi ya nyota moja na nusu akiwa amecheza mapambano 13 akishinda mara tisa na mawili ameshinda kwa 'KO' akipoteza mawili na moja kwa 'KO' na kutoka sare mara mbili.

Naye mpinzani wake Kunoga ambaye ni Zhetibayev ni bondia namba mbili kati ya mabondia watatu nchini kwao katika uzani wa 'bantam' huku Duniani akiwa wa 191 kati ya 1149 pia ni bondia mwenye hadhi ya nyota moja na nusu akicheza mapambano saba akishinda sita na manne kati ya hayo ni kwa 'KO' na kupoteza pambano moja.

Kila la kheri Kunoga nenda kaiwakilishe vyema Tanzania kwenye mchezo wa ngumi za kulipwa huko ughaibuni.
 

0/Post a Comment/Comments