CCM KUTAMBULISHA RASMI WAGOMBEA URAIS BARA NA ZANZIBAR

***


 Katibu Mwenezi na Itikadi CPA Amosi Makala amewataka wananchi wajitokezee kwa wingi katika kadhimisho miaka 48 ya Chama cha Mapinduzi (CCM) itakayo fanyika jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma, katika kuelekea kuadhimisho hayo, Makala amesema lengo kuu la sherehe hiyo ni kuwatambulisha mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Aidha, amesema kuadhimisha kwa miaka 48 tangu kuundwa kwa chama hicho kimekuwa imara na kinachotekeleza ilani yake ya Amani na Utulivu pamoja na uwepo wa vyama vya siasa.

Katika hatua nyingine, amewapongeza wakuu wa mikoa yote kwa kuzindua sherehe hizo katika mikoa mbalimbali, ambapo zitaisha tarehe 4 mwezi huu na baada ya hapo watakuja kujumuika nasi jijini Dodoma ambapo sherehe hiyo itafanyika tarehe 5 mwezi huu wa Februari.

0/Post a Comment/Comments