****
Na Lilian Lucas,Morogoro
Nchi za Tanzania na Japani kupitia Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la JICA zimezindua kigoda cha JICA chenye lengo la kubadilishana mawazo na uzoefu kati ya nchi ya Tanzania na Japan katika masuala ya mbalimbali ya kilimo hususaani kilimo cha Umwagiliaji.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kigoda hicho, Naibu makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Maulid Mwatawala,alisema lengo la serikali kuongeza kilimo cha umwagiliaji kwa asilimia 50 mpaka ifikapo 2030 hivyo uwepo wa kigoda hivho kutaleta tija zaidi.
Profesa Mwatawala alisema Kigoda cha JICA kina jukwaa la kuhakikisha wataalamu, watafiti wa kilimo katika nchi hizo mbili wanabadilishana uzoefu ambapo wameanza na suala la umwagiliaji.
Aidha alisema nchi ya Japan imepiga hatua kubwa kwenye masuala ya miundombinu ya umwagiliaji na teknolojia, hivyo SUA jukumu iliyopewaa ni taifa ni kuhakikisha wanafundisha wahandisi wa kilimo ambao watasaidi nchi kwenye maeneo mbalimbali kulingana na mipango iliyopo ukiwemo mpango wa jenga kesho iliyobora(BBT) ambayo itakuwa lengo la kuwa na wahandisi wa kilimo ambao watatoa utaalamu kwenye wilaya mbalimbali kwa kuchimba visima.
“Lakini katika agenda ya 1030 Wizara ya Kilimo inazungumzia kuongeza kilimo ch umwahiliaji kufikia hekta milioni nane na itasaidia ,”alisema.
Prof. Mwatawala alisema kwa kupata uzoefu kutoka kwa wataalamu chini Japan, mbinu bora zinahitajika kwa wingi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwani ongezeko la watu linahitaji wingi wa maji katika matumizi kama kunywa, chakula na mengineyo.
Alisema kwa miaka mingi Utafiti na Ugani vimekuwa havisomani,havikutani na kuanya wizara mbili ya Kilimo Na TAMISEMI zimeshirikiana kwenye program mbili zinazoendelea na zitaleta mafanikio makubwa kwa kubadilisha mfumo wa ugani, moja wapo ikiwa ni BBT Pamba pamoja na kwenye uzalishaji wa Pamba na kwamba vijana wengi waliajiriwa kutokana na program hizo wanatoka SUA.
`Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Tanzania Mikami Yoichi akizungumza alisema amefurahishwa na ushirikiano uliopo kati ya SUA na JICA na kwamba Japani itaendelea kusaidia kwenye kilimo hususani kilimo cha umwagiliaji,lakini ni matumaini yake kuwa uwepo wa Kigoda cha JICA utaleta tija katika suala zima la kilimo cha umwagiliaji nchini Tanzania.
Yoichi alisema pamoja na Japan kumleta mtaalamu mzoefu kwenye masula ya umwagiliaji kwa zaidi ya miaka 30,pia imekuwa ikichangia maendeleo na kutoa misaada kwenye maeneo mbalimbali.
“Tutaendele kutoa mbinu, elimu ya kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya kisasa kwa kutumia teknolojia hasa kwa wakulima wadogo,”alisema.
Akifungua mafunzo haya yaliyowakutanisha watafiti, maprofesa na wanafunzi kutoa chuo kikuu cha sokoine cha kilimo SUA Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Wilson Mahera alisema uwepo wa Kigoda hicho ni Fursa kwa nchi ya Tanzania na Japani kwani kuanzishwa kwa jukwaa hilo kutasaidia kuwakutanisha na kuwa na uwezo wa kufanya tafiti mbalimbali za kuweza kupata mbinu za kuwa na kilimo cha kisasa hasa kilimo cha umwagiliaji.
Mwisho.
Post a Comment