KCB BANK TANZANIA YASAINI MKATABA WA DOLA MILIONI 15 NA WATER EQUITY

KCB Bank Tanzania imesaini makubaliano na taasisi ya kimataifa ya WaterEquity wenye thamani ya Dola 15 milioni sawa na Shilingi 39.48 bilioni wenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa majisafi na usafi wa mazingira nchini.

Ubia huu umelenga kutoa ufadhili kwa wafanyabishara, viwanda na wakandarasi katika sekta ya maji waliopo chini ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Dar es Salaam (DAWASA) pamoja na Wakala wa Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini ubia huo, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Biashara wa Kanda wa KCB Group na Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank Tanzania, Paschal Machango ambaye ni Mkuu wa Idara ya Hazina -KCB amesema ubia huo ni muhimu katika kukuza biashara ya benki na kuchangia agenda ya maendeleo endelevu nchini.

KCB Bank imekuwa mstari wa mbele katika kuwezesha miradi ya maji nchini kwa kutoa mikopo na ufadhili kwa wafanyabishara na wakandarasi mbalimbali.

Kwa mwaka 2024, KCB Bank ilitoa zaidi ya USD milioni 28 sawa na Shilingi 72.8 bilioni kwa mikopo inayolenga miradi ya maji na usafi wa mazingira ikiwa ni pmaoja na sehemu ya ubia wetu na taasisi ya WaterEquity.

Kwa upande wake, Njeri Kirumbi, Mkuu wa Afrika wa Taasisi za Kifedha, WaterEquity alisema “Taasisi yetu ya WaterEquity inafuraha kuungana na KCB Bank katika kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama nchini.





 

0/Post a Comment/Comments