KUWASILISHA KAZI TUZO ZA UANDISHI TMDA MWISHO APRILI 18


***

Tausi Mbowe, Dar 

Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Yale Mashindano ya Uandishi ambao wameripoti habari za Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), sasa kujulikana hivi karibuni. 

Tuzo hizo zinazotolewa kila mwaka na mamlaka hiyo, zinafika tamati ya kuwasilisha kazi hizo Ijumaa Ijayo Aprili 18,2025.

Mapema mwezi uliopita Mamalaka hiyo ilitangaza kuanza kupokea kazi za waandishi waliofanya kazi za TMDA kwa upande wa Radio, Televisheni, Magazeti na mitandao ya kijamii. 

Taarifa ya Mamlaka hiyo iliyomnukuu Mkurugenzi Mkuu Dk Adam Fimbo ilisema kuwa kazi zitakazoshindaniwa ni za kuanzia Julai 2024 hadi Machi 

2025.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kazi zote zinapaswa kuwasilishwa 

ifikapo au kabla ya Aprili 18,2025.

Dk Fimbo alisema lengo la Tuzo hizo ni kutambua mchango wa waandishi wa habari na kuleta hamasa katika kuelimisha jamii kuhusu masuala ya udhibiti wa dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi.

0/Post a Comment/Comments