MBUNGE WA IGALULA ATIMIZA AHADI YAKE


 ****

Leo Tarehe 22/02/2025 *Mbunge Wa Jimbo la Igalula Mhe. Venant Protas* ameendelea na Ziara katika Kata ya Tura na kufanya Mambo yafuatayo :-

1)Amekutana na viongozi Wa Halmashauri kuu  Ya CCM ya Kata ya Tura pamoja na Maborozi wote Katika Kata ya Tura pamoja na mambo mengine Mhe Venant Daud amechangia *mifuko 50 ya cement yenye Thamani ya Tsh 1,100,000* Kwa ajiri ya ujenzi wa ofisi ya  CCM Kata ya Tura.

2)Mhe Mbunge amefanya Mkutano Wa hadhara katika Kijiji cha Tura Kwa lengo la kusikiliza Kero katika mkutano huo Mhe Mbunge amewachangia wananchi *sement mifuko 50 yenye Thamani ya Tsh 1,100,000.amechangia Bati 60 yenye Thamani ya Tsh 2,250,000 pia amewachangia milioni 5* Kwa ajiri ya ujenzi Wa Kituo cha Police Tura.katika Hatua nyingine kupitia mkutano huo wa Hadhara Mhe Mbunge amewachangia bodaboda kiasi cha *Tsh 1,000,000* Kwa Ajili ya ujenzi Wa Banda la bodaboda la kupumzikia 

Ziara itaendelea kesho Kwa kukutana na viongozi Wa Umoja vijana Jimbo la Igalula

 _Imetolewa na ofisi ya Mbunge Jimbo la Igalula_

0/Post a Comment/Comments