Mradi wa ujenzi wa matenki ya hifadhi ya mafuta katika eneo
la Kigamboni, jijini Dar es Salaam, umefikia asilimia 14.77. Mradi huu
unajumuisha ujazaji na ushindiliaji wa kifusi ili kuwezesha uhifadhi bora wa
mafuta.
Akizungumza wakati wa ziara yake kwenye mradi huo, Waziri wa Uchukuzi, Profesa
Makame Mbarawa, amesema lengo la mradi ni kuondoa changamoto za meli za mafuta
kusubiri kwa muda mrefu bandarini kutokana na uchache wa matenki ya hifadhi
yaliyopo.
Kuhusu ufanisi wa bandari, Prof. Mbarawa amesema umeimarika, ambapo mapato ya
sekta binafsi yameongezeka na kufikia wastani wa shilingi bilioni 440 katika
miezi sita iliyopita. Aidha, muda wa kushusha mizigo ya makasha umepungua
kutoka siku saba hadi siku tatu tangu kampuni ya DP World kutoka Dubai ilipoanza
kazi.
Kwa upande wake, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania
(TPA), Mhandisi Baraka Mdima, amesema watahakikisha mradi huo unatekelezwa kwa
viwango bora.
Mradi huu unagharimu shilingi bilioni 678.76 na unahusisha ujenzi wa matenki
15. Kati ya hayo, matenki sita yatatumika kuhifadhi dizeli, matano petroli,
matatu kwa mafuta ya ndege, huku tenki moja likitumika kuhifadhi mafuta ya
akiba. Mradi wa ujenzi wa matenki ya hifadhi ya
mafuta katika eneo la Kigamboni, jijini Dar es Salaam, umefikia asilimia 14.77.
Mradi huu unajumuisha ujazaji na ushindiliaji wa kifusi ili kuwezesha uhifadhi
bora wa mafuta.
Akizungumza wakati wa ziara yake kwenye mradi huo, Waziri wa Uchukuzi, Profesa
Makame Mbarawa, amesema lengo la mradi ni kuondoa changamoto za meli za mafuta
kusubiri kwa muda mrefu bandarini kutokana na uchache wa matenki ya hifadhi
yaliyopo.
Kuhusu ufanisi wa bandari, Prof. Mbarawa amesema umeimarika, ambapo mapato ya
sekta binafsi yameongezeka na kufikia wastani wa shilingi bilioni 440 katika
miezi sita iliyopita. Aidha, muda wa kushusha mizigo ya makasha umepungua
kutoka siku saba hadi siku tatu tangu kampuni ya DP World kutoka Dubai
ilipoanza kazi.
Kwa upande wake, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania
(TPA), Mhandisi Baraka Mdima, amesema watahakikisha mradi huo unatekelezwa kwa
viwango bora.
Mradi huu unagharimu shilingi bilioni 678.76 na unahusisha ujenzi wa matenki
15. Kati ya hayo, matenki sita yatatumika kuhifadhi dizeli, matano petroli,
matatu kwa mafuta ya ndege, huku tenki moja likitumika kuhifadhi mafuta ya
akiba.

Post a Comment