PAKAYA YAWAKUTANISHA WATENDAJI WA SERIKALI KIBITI,YASISITIZA UHIFADHI MIKOKO

Mkurugenzi wa Mipango na Uchumi wa Taasisi ya Pakaya Culture Environmental Groups Bakari Hassan Kisoma akitambulisha Miradi wanayoitekeleza katika Kikao kazi na Maafisa watendaji wa serikali Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani ambacho kimeratibiwa na PAKAYA.

Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la PAKAYA Abdallah Ally Pendekezi akisoma risala katika Kikao kazi na Maafisa watendaji wa serikali Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani ambacho kimeratibiwa na PAKAYA.

Afisa Tarafa wa Wilaya ya Kibiti Salum Maganya akizungumza katika Kikao kazi na Maafisa watendaji wa serikali Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani ambacho kimeratibiwa na PAKAYA.

Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la PAKAYA Abdallah Ally Pendekezi (kulia) pamoja na Afisa Tarafa wa Wilaya ya Kibiti Salum Maganya (kushoto) wakiongoza Kikao kazi na Maafisa watendaji wa serikali Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani ambacho kimeratibiwa na PAKAYA.

  

Baadhi ya watendaji wa serikali ambao wameshiriki katika katika Kikao kazi na Maafisa watendaji wa serikali Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani ambacho kimeratibiwa na PAKAYA.

..........................

NA MUSSA KHALID KIBITI PWANI

Shirika lisilokuwa la Kiserikali la PAKAYA Culture Environmental Groups (PCEG) limewasisitiza watendaji wa serikali katika Wilaya ya Kibiti kuonyesha ushirikiano kwa Shirika hilo ili liweze kufanikisha kwa wakati utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kuhamasisha uhifadhi shirikishi na utumiaji endelevu wa rasilimali mikoko na bioanuai wanayoitekeleza katika Wilaya hiyo.

Hayo yamejiri Leo katika Kikao kazi na Maafisa watendaji wa serikali Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani ambacho kimeratibiwa na PAKAYA kwa Lengo la kujadili namna ya kuendeleza jamii na Mazingira katika Delta ya Rufiji Wilayani humo Ili kuondoa umaskini kwenye jamii.

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la PAKAYA Abdallah Ally Pendekezi amesema lengo lao ni kuhakikisha wanaimarisha uhifadhi wa pamoja wa misitu ya mikoko na bioanuai nyinginezo mpaka kufikia January 2026 mikoko 60,000 iwe imetolewa.

Aidha amewasihi madiwani na watendaji katika Wilaya hiyo kuendelea kuonyesha ushirikiano kwa Shirika hilo ikiwa ni pamoja na kutosababisha vikwazo pindi wana PAKAYA wanapokuwa kwenye majukumu yao katika Kata ambazo wanaziongoza.

"Mradi huu dhamira yake ni kueneza na kuendeleza falsafa ya uhifadhi shirikishi na utumiaji endelevu wa rasilimali,ili kuchangia juhudi za Kimataifa,Kitaifa na za kijamii kuhakikisha njia sahihi na madhubuti za kuhifadhi Bioanuai na vipaumbele vya Maendeleo endelevu na kuboresha jamii zinatekelezwa" amesema Pekendezi

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika kikao hicho Afisa Tarafa wa Wilaya ya Kibiti Salum Maganya amelipongeza Shirika hilo kwa kuonyesha jitihada mbalimbali katika kuhamasisha upandaji wa mikoko jambo ambalo limekuwa likiimarisha uhifadhi wa mazingira na kuongeza uoto katika Wilaya hiyo.

‎"Sisi binadamu huwa tunakata mikoko halafu kuna Taasisi kama hii PAKAYA zinakuja zinatutengenezea hivyo tuonyeshe ushirikikishi kwa watu ili nao wahamasike zaidi kuepuka kuharibu mazingira"amesema Maganya

Awali,Mkurugenzi wa Mipango na Uchumi wa Taasisi ya Pakaya Culture Environmental Groups Bakari Hassan Kisoma amevitaja vijiji vinavyofikiwa na mradi huo kuwa ni pamoja katika vijiji Kiongoroni,Jaja,Pombwe,Ruka,Mbuchi,Mbwera(E),Mbwera (W),Kyechuru,Msala,Maparoni,Nyamisati na Kiomboni.

Amesema pia wanaendeleza ufugaji wa Nyuki na kuanzisha utalii wa Ikolojia kuwa shughuli mbalimbaliza kiuchumi kufikia malengo 2026.

‎Pia mkakati Mwingine ameutaja kuwa ni kutatua migogoro ya matumizi ya mikoko na bioanuai nyinginezo na kutoa njia mbadala kwa kuwashirikishs wadau wote.

Kwa upande wao baadhi ya wadau walioshiriki katika kikao hicho akiwemo Afisa Tarafa Kikale Salim Mohammed pamoja na Jesca Kaduma kutoka Salale wameipongeza PAKAYA kwa kuendelea kuonyesha jitihada za kuimarisha utunzaji wa mazingira kwenye maeneo yao.

Aidha wamesema wataendelea kuonyesha ushirikiano kwa Taasisi hiyo Ili iweze kufanikisha malengo iliyojiwekea ya kuhamasisha uhifadhi wa matumizi endelevu ya misitu ya mikoko na bioanuai nyinginezo kwa ajili ya kuendeleza jamii na kupunguza umaskini katika Wilaya ya Kibiti kufika Januari 2026.

Mradi huo unaotekelezwa na Shirika la PAKAYA unafadhiliwa na Program ya Ruzuku ndogo za mfuko wa mazingira Duniani,(GEF SGP) inayotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

0/Post a Comment/Comments