RAIS SAMIA AMSHUKURU UMMY MWALIMU UJENZI WA HOSPITALI HANDENI

 

****

Na: Mwandishi Wetu, Tanga

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Ummy Mwalimu, kwa utendajikazi wake alipokuwa Waziri wa Afya ulioacha alama ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Rais Samia ameyasema hayo Februari 23, 2025, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Tanga akianzia wilaya ya Handeni ambapo amesema Ummy Mwalimu amefanya kazi kubwa ambayo imekuwa chachu ya mafanikio ya ujenzi wa hospitali hiyo.

"Lakini hapa nataka niseme jambo, Tanga oyee, Tanga nataka niseme jambo, kazi hii yote imefanyika na kwa dhati nataka nimshukuru sana mdogo wangu Odo Ummy (Ummy Mwalimu). Kazi hii (ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Handeni) tuliianza nae na imefika vizuri hadi pale alipokabidhi kijiti kwa Mheshimiwa Jenista ambaye tunaendelea nae. Kwahiyo Odo Ummy, ahsante sana, umefanya mchango wako kwa kiasi kikubwa na Mungu atakulipa fungu lako," amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema licha ya hospitali hiyo kuwa ya wilaya lakini ina hadhi ya hospitali ya mkoa huku akiwakumbusha wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wake, imeupatia mkoa huo shilingi Trilioni 3.1 za kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo na hivyo yuko mkoani huko kujionea miradi hiyo.









0/Post a Comment/Comments