Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kumrejesha kwake
aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Januari
Makkamba.
Akizungumza mjini Lushoto leo ikiwa ni muendelezo wa
ziara yake ya siku saba mkoani Lushoto, Rais Samia alimuita mbele waziri huyo
wa zamani na mbunge wa Bumburi na
kutangaza kumrejesha rasmi kwake kisha kumkumbatiam
"Kabla sijamaliza hotuba yangu naomba nimuite
mwanangu Januari aje huku. Sisi wamama mtoto wako akikosea unampiga kofi na
mkumfichia chakula hivyo ndivyo nilivyofanya lakini leo natangaza rasmi
namrejesha tena huku, " alisema Rais Samia huku akimkumbatia mbunge huyo.
Awali katika salamu zake kwa niaba ya wananchi wa
Bumburi, Makamba alimshukuru Rais Samia kwa kumuamini na kumteua kuongoza
wizara mbalimbali.
Kwa mujibu wa Makamba, Rais Samia alimuamini na
kumteua kuwa waziri lakn kabla ya uteuzi huo alipata kufanya kazi akiwa naibu
waziri wa wizara ya Muungano ambayo waziri wake alikuwa Samia Suluhu Hassan
ambaye ndiye alimfundisha kazi ya uwaziri.
"Hivi unavyoniona leo ni matunda yako muheshimiwa Rais. Nilipata kufanya kazi wizara moja na wewe ndiyo ulikuwa waziri wangu na mimi msaidizi wako, wewe ndiyo ulinifundisha uwaziri kwahiyo kama kuna nilipatia na kuna matunda basi maua haya ni yako. Napenda kukushukuru sana mheshimiwa Rais kwa kuniamini na kunipa nafasi kuongoza katika Serikali yako kama waziri.
Post a Comment