Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Feb 18,2025
Baadhi ya wanahabari jijini Dododa ambao wameshiriki kwenye mkutano wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha leo feb 18,2025
......................
Na Ester Maile _Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa kielelezo cha mafanikio makubwa yanayoendelea katika sekta ya michezo kwa kuhamasisha na kuweka mazingira mazuri ya michezo nchini.
Hayo yameelezwa leo 18/Februari 2025 na
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
Ameongeza kuwa, Rais Samia ameleta mabadiliko kwa vitendo ambayo yameongeza ufadhili, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kisasa ikiwemo ukaranbati wa uwanja wa BENJAMIN MKAPA.
Ametaja mafanikio mengine kuwa Tanzania imekuwa mwenyeji wa matukio makubwa ya michezo ya Kimataifa, kuondoa kodi kwa nyasi bandia, Tanzania kuwa Makao Makuu ya Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Afrika Kanda ya Tano na kuanzishwa kwa Mfuko wa Michezo.
Vile vile, Tanzania kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia, kuanzishwa kwa mfumo wa usajili wa Vyama na Vilabu wa kidijitali "SARS", kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa pamoja na timu za Tanzania kufuzu mashindano ya kimataifa.



Post a Comment