RAIS WA TLS AISHAURI SERIKALI SAKATA LA BANDARI BAGAMOYO

****

Na Mwandishi wetu

Ni baada ya serikali kukanusha vikali madai ya uwekezaji wa bandari ya Bagamoyo kwa kampuni ya Saudia Arabia,rais wa Chama Cha wanasheria Tanganyika(TLS) Wakili, Boniface Mwambukisi, ameishauri serikali kuweka mambo hadharani ili kuondoa sintofahamu kwa Umma. 

Kwa mujibu wa Mwambukusi, kwa kuzingatia umuhimu wa bandari ya Bagamoyo ni muhimu kwa Waziri mwenye dhamana kuhakikisha kwamba katika maeneo yote yanayogusa uwekezaji kwenye Mali Asili za Tanganyika miradi yote au tenda ziwe wazi kwa umma ili kujua kinachoendelea na zaidi.

"Maelezo ya mikataba, hati za makubaliano (MoUs), au makubaliano yoyote katika hatua zote yafanyike kwa Uwazi"

2. Asili na upeo wa ushiriki wa wadau katika miradi hii ikiwa ni pamoja na ahadi zozote za kifedha, kiutendaji, au kisera ziwekwe wazi kwa umma kuimarisha uwajibikaji" amesema Mwambukusi

Kadhalika amependekeza ripoti za upembuzi yakinifu, tathmini ya athari za kimazingira, au uchambuzi wa kiuchumi uliofanyika kuhusu maendeleo au ushirikiano wa ubia wa miradi ya umma iwe wazi badala ya kificho.

Amesema utaratibu wa ushirikishwaji wa wananchi na mashauriano ya umma yanayofanyika au yanayotarajiwa kufanyika ni muhimu kuhakikisha uwazi na ushirikiano unakuwepo kwa maslahi ya raslimali za nchi.

"Mfumo wa kisheria na wa udhibiti unaosimamia makubaliano haya na marekebisho yoyote yaliyofanywa au yanayopendekezwa ili kuwezesha ushiriki wa wawekezaji wa kigeni katika maeneo ya raslimali asili ni lazima yawekwe wazi na yaboreshwe zaidi" amesema Mwambukusi.


 

0/Post a Comment/Comments