Benki ya Selcom Microfinance Tanzania Limited imezindua
rasmi SELCOM PESA, huduma ya kifedha ya kidigitali inayolenga kutoa suluhisho
rahisi, salama, na nafuu kwa Watanzania.
Kupitia teknolojia ya kisasa na mfumo wa TIPS, huduma hiyo inawawezesha
watumiaji kufanya miamala ya kifedha kwa gharama nafuu, ikiwa ni pamoja na
uhamishaji wa fedha kati ya benki na mitandao ya simu, malipo ya bili, na
malipo ya Serikali kupitia GePG.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba,
ambaye alisisitiza umuhimu wa teknolojia katika kuimarisha ushirikishwaji wa
kifedha na kupunguza gharama za miamala kwa wananchi.
Uzinduzi huu umeambatana na kampeni maalum ya “5 kwa Jero”, inayoruhusu wateja
kufanya miamala mitano kwa siku kwa Sh500 tu, hatua inayolenga kupunguza
gharama za kifedha kwa wananchi wa kipato cha chini.
Huduma ya SELCOM PESA inapatikana kupitia Google Play na App Store, ikiwa ni
sehemu ya juhudi za Selcom Microfinance Tanzania kuleta mapinduzi katika sekta
ya kifedha na kuhakikisha huduma za kifedha zinakuwa nafuu na zinazopatikana
kwa urahisi kwa Watanzania wote.
Post a Comment