Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
Mkoa wa Kinondoni imebaini mapungufu madogo katika miradi mwili yenye thamani
ya Shilingi Millioni 144,800,000 iliyohusu sekta ya elimu na Ujenzi.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu
wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni Christian Nyakizee wakati akitoa taarifa ya
utendaji kazi kwa kipindi cha Octoba hadi Disemba 2024.
Nyakizee amesema katika kipindi hicho wamefuatilia
miradi mitano yenye thamani ya Shs Bill 2.85 huku miwili ikikutwa na mapungufu
na hivyo kuwashauri wahusika kufanya marekebisho.
‘Mradi wenye thamani ya milioni tisini ulibainika
kubadilishwa kazi iliyotolewa kibali awali ambapo kilikuwa ni cha kufanya
ukarabati wa majengo ya madarasa lakini badala yake wakaanzisha ujenzi wa
madarasa mapya’amesema Nyakizee
Aidha Mkuu huyo wa TAKUKURU (M) Kinondoni amesema
katika kipindi hicho wamepokea malalamiko 85 ambapo kati ya hayo 46 lihusu
Rushwa na 39 hayakuhusu rushwa.
Amesema kuhusu malalamiko ambayo hayakuhusu rushwa
walalamikaji wengine wameshauriwa na majalada kufungwa na wengine wameelezwa
sehemu sahihi ya kupeleka malalamiko yao.
Katika hatua nyingine Nyakizee amesema wamejipanga
kuendelea kuhamasisha wananchi kushirikiana na TAKUKURU wakati wa maandalizi ya
uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa Madiwani,Wabunge na Rais.
‘TAKUKURU tutaendelea kupokea malalamiko yote
yanayohusu rushwa na kuyafanyia kazi kwa uharaka ili kuweza kudhibiti vitendo
vyote vya rushwa katika wakati wote’ameendelea kusisitiza Nyakizee
Hata hivyo imeendelea kuwasisitiza na kuwakumbusha watumishi kuzingatia misingi ya maadili ya utumishi wa umma katika kutekeleza majukumu yao bila kujihusisha na rushwa kwani inanyima haki

Post a Comment