BILIONI 381 ZAKAMILISHA UJENZI MADARAJA TISA SERIKALI AWAMU YA SITA

Mkurugenzi wa Mipango ya miundombinu ya Wakala wa barabara Tanzania( TANROAD) Mhandisi Ephatar Mlavi akizungumza na waandishi wa wahabari jijini Dodoma leo tar 17/2/2025
.................

Na Ester Maile Dodoma

Kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita madaraja tisa yamekamilika kwa gharama ya shilingi bilion 381.301na mengine kumi ujenzi wake unaendelea kwa gharama ya shilingi bilion 985.802 huku madaraja kumi na tisa yapo katika harakati za kuanzishwa ujenzi.

Akieleza hayo mbele ya waandishi wa habari leo 17 februari 2025 jijini Dodoma Mkurugenzi wa Mipango ya miundombinu ya Wakala wa barabara Tanzania( TANROAD) mhandisi Ephatar Mlavi amesema kuwa katika ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje katika jiji la Dodoma yenye jumla ya urefu wa kilomete 112 hadi kufikia Februari 2025 ujenzi umefikia asilimia 91sehemu ya kwanza ya Nara,Veyula ,Mtumba ,na lhumwa mpaka bandari kavu kilomete 5.3 na asilimia 85 kwa sehemu ya pili ya lhumwa bandari kavu matumbulu na Nara kilomite 62.

Nae Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa serikali Gerson Msigwa amevitaka vyombo vya habari kutumia fursa hii ya mikutano kuwapa taarifa watanzania kuhusu miradi mbalimbali inayo tekelezwa na serikali ya awamu ya sita. 

Mwisho Msigwa amesisitiza taasisi za umma kuja kutoa taarifa za utendaji wa taasisi kwa kipindi cha miaka minne.

0/Post a Comment/Comments