TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRICA ZINAZOZALISHA KAHAWA

*******

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa wa wakuu wa nchi za Afrika zinazozalisha Kahawa unaotarajia kufanyika Februari 21 na 22, 2025 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amewataka watanzania kutumia fursa mbalimbali za kibiashara kuweza kuinua vipato vyao kupitia mkutano huo

RC Chalamila ameyasema hayo leo wakati akizungumza waandishi wa habari ambapo amesema kufuatia kuwepo kwa mkutano huo utakaofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwl Julius Nyerere (JNICC) zipo fursa nyingi za kiuchumi hivyo ni muhimu kwa watanzania kutumia vizuri fursa hiyo.

Aidhaa Rc Chalamila amesema Mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika zinazozalisha Kahawa utafanyika februari 22,2025 ukitanguliwa na mkutano wa mawaziri wa kilimo kwa nchi za Afrika zinazozalisha Kahawa utakaofanyika februari 21,2025 hivyo amewataka wakulima na wafanyabiashara wa Kahawa kutumia mkutano huo kuonesha bidhaa zao

Vilevile akizungumzia suala la Barabara RC Chalamila amesema kuwa kwa kipindi hiki barabara hazitofungwa isipokuwa kwa barabara ya kutokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere kuelekea mjini ndio imewekewa utaratibu maalum ambapo magari bajaji na pikipiki havitaruhusiwa kupita kwenye barabara ya mwendokasi kwa kuwa barabara hiyo itatumiwa na wageni wanaokuja nchini.

Mwisho RC Chalamila amesemaTanzania imefanikiwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na uongozi imara na mzuri wa Rais Dkt Samia unaoleta utulivu wa kisiasa, amani pamoja na ulinzi na usalama madhubuti.





 

0/Post a Comment/Comments