*****
Chama cha Wafanyakazi Tanzania (TUICO, kimesain Mkataba wa Hali Bora za Kazi kwa watumishi wake.
Akizungumza jana, Februari 10, 2025, jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla hiyo, Mwenyekiti wa TUICO, Paul Sangeze, amewataka watumishi wote kuchapa kazi kwa bidii ili kuhakikisha makubaliano hayo yanatekelezeka.
Aidha, TUICO imewataka wanachama wake kujipanga vizuri kwa ajili ya uchaguzi wa chama hicho, ili kuchagua viongozi watakaolinda maslahi na uhai wa chama.
“Mwaka huu ni wa uchaguzi wa TUICO. Hakikisheni mnapata viongozi bora, Uchaguzi usiwe wa kupitisha wagombea bila kupingwa, hata kama mgombea ni mmoja, kura za ‘Ndiyo’ au ‘Hapana’ ni muhimu,” alisema Sangeze.
Hata hivyo, ameeleza kuwa katika mwaka mmoja uliopita, chama kimefanikiwa kuongeza wanachama 15,032, kufunga mikataba 98 ya hali bora, na kushinda migogoro 214 kati ya 303 iliyopokelewa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Sekta ya Biashara TUICO, Willy Kibona, alisema mkataba uliosainiwa utaimarisha maslahi ya wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na waajiri kugharamia matibabu na misaada kwa wafanyakazi wanaopata madhara kazini.
Naye Katibu Msaidizi wa TUICO Kigamboni, Hamisa Simba, alisisitiza mshikamano wa wafanyakazi, akisema mkataba huo uwe chachu ya kuongeza tija na ufanisi mahali pa kazi.
Post a Comment