*******
Umoja wa Maimamu Tanzania UMATA umeiomba serikali kuajiri walimu wa masomo ya Dini kutokana na masomo hayo kurasimishwa na Kuingia katika mtaala wa masomo katika ngazi mbalimbali hapa nchini.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar Es Salaam, Mratibu wa umoja huo Alhaji Juma Nchia Amesema kuwa kurasimishwa kwa masomo ya Dini kutaongeza Wigo wa ajira na kuchochea hamu ya Wanafunzi kujifunza masomo ya dini zao ili kuwa na vizazi vyenye imani thabiti na uadilifu
Amesema uwepo wa masomo ya dini utasaidia wanaoma kuwa na nidhani ambayo itapunguza Rushwa na kuleta hofu ya Mungu ambapo pia ameiomba serikali kurasimisha kwa masomo hayo katika ngazi ya Shule za Msingi.
Katika hatua nyingine akizungumzia wajibu wa umoja huo katika kukuza maslahi ya maimamu nchini katibu mkuu wa UMATA Taifa Amir Khamis Mbwana amesema umoja umeandaa mkutano mkuu wa pili unaotarajiwa kufanyika February 15 na 16 mwaka huu lengo likiwa ni kutengeneza muongozo wa maimamu nchini
Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa UMATA
Hussein Mchomolo amesema kuwa mkutano huo utatoa fursa kwa maimamu nchini
kujadili namna bora ya kujiimarisha kiutendaji sambamba na kusimamia misingi ya uongozi na utawala
bora
Post a Comment