Ikiwa imetimu mwaka mmoja na miezi sita tangu soko la mabibo ndizi kukabidhiwa kwa Manispaa ya Ubungo, leo tarehe 10 Februari 2025 viongozi wapya waliochaguliwa na wafanyabiashara wa soko hilo wameapishwa na kupata semina elekezi tayari kwa kuanza kutekeleza majukumu yao katika soko hilo.
Viongozi hao ambao ni Wenyeviti, Makatibu na Wajumbe wamechaguliwa katika vitengo sita vinavyopatikana katika soko hilo ambavyo ni kitengo cha Ndizi, Viazi na Vitunguu, Matunda, Nyanya, mbogamboga pamoja na kitengo cha Mama na Baba lishe
Akiongea wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo, Mkuu wa Idara ya viwanda, uwekezaji na biashara Manispaa ya Ubungo Bi. Mary Mwakyosa amewapongeza viongozi hao kwa kuchaguliwa na wafanyabiashara wa soko hilo na kuwasihi kuwa dhamana walioyopewa ya kusaidia uendeshaji wa soko ni kubwa hivyo wazingatie sheria kanuni na miongozo katika kutekelezaji wa majuku yao huku wakizingatia maslahi ya wafanyabiashara na serikali.
Mwakyosi amewaleza kuwa “Ukiwa kiongozi, wewe ni daraja kati ya wafanyabiashara na serikali hivyo mtatakiwa kusimamia na kutatua matatizo na migogoro ya wafanyabiashara kwa kuzingatia mipaka yenu, na mgogoro ukikushinda wasilisha ofisi ya Meneja kwa hatua zaidi”
Kwa upande wake wakili Coletha Mushi amewaeleza viongozi hao wapya kuwa katika utendaji wao wa kazi wanapaswa kutenda haki katika majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo “na kitendo cha kuapa kinaashiria kuwa upo tayari kufanya kazi kwa mujibu wa sheria”
Akiongea kwa niaba ya viongozi wenzake baada ya mafunzo na kiapo, Mwenyekiti wa kitengo cha Baba na Mama lishe Bi Mariamu Self ameishukuru Manispaa kwa kuendesha uchaguzi wa huru na haki na viongozi tuliochguliwa tunaahidi kwenda kutekeleza majuku yetu kwa kuonesha ushirikiano mzuri kwa wafanyabiashara wenzetu na Meneja wa soko huku tukizingatia sheria, kanuni na miongozo







Post a Comment