WAGONJWA WA SELIMUNDU TANZANIA KUTIBIWA KWA TEKNLOJIA MPYA


 ****

Serikali imeeleza kuwa imeanza kufanya matayarisho ya wataalam na teknolojia mpya ya matibabu ya ugonjwa wa selimundu inayojulikana kama CRISPR Cas 9 Technology (Gene Editing).

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi Februari 6, 2025 na Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kawe (CCM), Josephat Gwajima aliyetaka kujua ni lini Serikali itaanza matibabu ya wagonjwa wenye selimundu kwa kutumia Crispr Gene Editing Technology.

Cc Mwananchi Digital 

0/Post a Comment/Comments