CCM YAPITISHA UKOMO WA VITI MAALUMU


 *****

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekubali kuweka ukomo wa vipindi vya udiwani na ubunge wa viti maalumu, ambapo uongozi huo hautazidi vipindi viwili (miaka 10).

Uamuzi huu wa CCM, ambao utaanza kutekelezwa mwaka 2030, ulifikiwa katika kikao cha Halmashauri Kuu kilichofanyika jijini Dodoma tarehe 10 Machi, 2025, chini ya Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.

Katibu wa Oganaizesheni wa CCM, Issa Haji Ussi, alitoa taarifa hii leo, Jumanne, 11 Machi, 2025, akisema kikao hicho kilijadili na kupokea agenda mbili: mapendekezo ya marekebisho ya kanuni za uteuzi wa wagombea uongozi katika vyombo vya dola kwa toleo la 2022, pamoja na Rasimu ya Ilani ya CCM kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025-2030.



0/Post a Comment/Comments