Serikali ya Awamu ya Sita, imesema usajili wa kazi zinazolindwa na Sheria ya hakimiliki na hakishiriki imeongezeka kwa 70% ambapo kuanzia mwaka 2021 mpaka Februari 2025, COSOTA, imesajili kazi za Sanaa na Uandishi 11,519 na Wabunifu 3,436.
Katika kipindi hicho, kamati maalumu ya Usajili ndani ya COSOTA inayojihusisha na masuala ya usajili, imefanikiwa kutoa mafunzo na ufafanuzi kuhusiana na hakimiliki kwenye kazi zilizopokelewa kwa idadi ya wabunifu 167.
Afisa Mtendaji Mkuu na msimamizi wa Hakimiliki(COSOTA) Doreen Sinare ameeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wahabari jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya COSOTA ndani ya kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na RAIS Dkt Samia Suluh Hassan.
Vilevile,COSOTA imetoa jumla ya vyeti 7,679 vya uthibitisho wa umiliki wa hakimiliki kwa wabunifu waliosajili kazi zao.
Amesema kwa mwaka 2021/ 2025, COSOTA imefanikiwa kufanya migao miwili, ukiwemo ambao ulikuwa ni mgao wa 23 uliofanyika tarehe 28/01/2022 na ulikuwa wa kiasi cha shilingi 312,290,259,000, ambapo Wasanii 1,123 walinufaika, na ulitokana na matumizi ya kazi 5,924 za muziki zilizotumika katika vituo 11 vya
Aidha amesema tarehe 21/07/2023 ulifanyika mgao wa 24 wa mirabaha kwa kazi za muziki ambapo COSOTA iligawa kiasi cha shilingi 396,947,743.20 na wasanii wa muziki 8,165 walinufaika kupitia kazi zao 61,490.
Amesema hivyo ni iwango vikubwa zaidi kuwahi kufanyika katika migao ya mirabaha ambayo COSOTA imekuwa ikigawa kwa miaka ya nyuma kabla ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita ambao ulianzisha kampeni ya kusisitiza watumiaji wa kazi za Sanaa katika maeneo ya biashara kulipia matumizi ya kazi
Mradi huo umewezesha COSOTA kupata ufadhili kwa ajili ya kutoa elimu ya uharamia na hakimiliki kwa kazi za ubunifu, ili kuweza kuboresha mfumo wa COSOTA, BASATA na TFB ili iweze kusomana.
Kwa kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita, COSOTA ilipokea jumla ya migogoro 136 na kusuluhisha migogoro 118. Migogoro 10 kati ya hiyo haikumalizika na ilifunguliwa kesi mahakamani na migogoro 8 inaendelea COSOTA. Sambamba na migogoro hiyo, COSOTA imehusika na kesi za hakimiliki 10.
COSOTA ilifanikiwa kuendesha semina ya kujengeana uwezo kuhusu masuala ya hakimiliki na Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki kwa makundi mbalimbali wakiwepo mahakama, bunge, wahariri, vyuo vikuu, mashirikisho na vyama vywa waandishi na wasanii na mawakili wasio wa serikali.
Kumekuwa na kuimarika kwa mahusiano na mashirika ya kimataifa yaliyochangia kupelekea utaratibu mahususi wa kuanzishwa kwa Kituo cha kutoa Elimu ya Hakimiliki.
Post a Comment