DAWASA YAJA NA MKAKATI KUFIKIA LITA BILION 2.1 IFIKAPO 2050

*****



Na Ester Maile _Dodoma 

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imejipanga kutekeleza miradi mbambali ya maji ili kukidhi mahitaji ya maji lita bilioni 2.1 kwa siku ifikapo mwaka 2050. 

Kaimu Mkurugenzi wa  Mamlaka hiyo ameeleza hayo leo jijini Dodoma katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu mafaniko ya mamlaka hiyo kwa kipindi cha miaka minne.

 Bwire ameeleza kuwa ni lazima kuwe na mipango ya muda mrefu ya kukidhi mahitaji ya maji ya maeneo yanayohudumiwa na DAWASA kwani kwa sasa ni mita za ujazo 685.6 lakini kutokana na kasi kubwa ya ongezeko la watu pamoja na viwanda, mahitaji ya maji lazima yazingatiwe hivyo DAWASA imeangalia mahitaji ya maji ya leo, na  miaka 10 ijayo, hadi ya mwaka 2050.


 Vile vile kuna  vyanzo vikubwa vya maji vilivyopo chini ya ardhi ni asilimia 7 na juu ya ardhi ni asilimia 93. Vyanzo vya juu ya ardhi ni mto Ruvu unaochangia asilimia 87, mto Wami unachangia asilimia 4 na Mtoni asilimia 2 ambapo vyanzo hivyo vinazalisha lita milioni 534.6.

Katika jitihada za kupunguza utegemezi wa maji juu ya ardhi, Mhandisi Bwire amesema Serikali imefanya kazi kubwa katika kuhakikisha maji chini ya ardhi yanapatikana ambapo imeanza  kuchimba visima virefu zaidi ya mita 600 katika maeneo ya Kigamboni lengo likiwa ni kusaidia pale ambapo maji juu ya ardhi yanapokuwa na changamoto kuwe na mbadala wa upatikanaji wa maji.




 

0/Post a Comment/Comments