DK FIMBO AFANYA ZIARA VIWANDA VYA DAWA

****

Tausi Mbowe

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Dk Adam Fimbo amefanya ziara katika viwanda kadhaa vya dawa vilivyopo jijini Dar es Salaam. 

Lengo la ziara hiyo ni kusikiliza changamoto zao za usajili wa dawa nchini zinazowakabili. 

Dk Fimbo alifanya ziara katika viwanda hivyo mapema leo Ijumaaa Machi 28, 2025.

Viwanda alivyotembelea ni pamoja na Kiwanda cha Dawa cha Mansoor Daya na Alfa vyote vya jijini Dar es Salaam. 

Katika ziara hiyo Mkurugenzi Fimbo aliambatana na maafisa mbalimbali wakiwamo wakurugenzi wa Mamlaka hiyo ili kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi.




 

0/Post a Comment/Comments