DKT FIMBO: WATANZANIA ACHENI KUTUMIA DAWA KIHOLELA

******

Na Tausi Mbowe

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imewataka Watanzania kuacha kutumia dawa kiholela bila kufuata maelekezo na ushauri wa wataalam wa afya. 

Mamlaka hiyo imesisitiza matumizi sahihi ya dawa ili kupunguza tatizo la usugu wa maradhi. 

Kauli hiyo imetolewa leo Julai 9, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt Adam Fimbo akizungumzia na waandishi wa habari.

"Usugu wa dawa limekuwa ni tatizo katika sekta yetu ya afya sasa, siku hadi siku tatizo hili linaongezeka kwa kasi, watu wananua dawa kiholela na kutumia bila kufuata ushauri, " alisema Dk Fimbo. 

"Sasa ni kawaida kwa mtu anayejisikia kichwa kinamuuma au chochote kwenda duka la dawa na kununua dawa ya kutuliza maumivu, wengine wanakwenda mbali zaidi na kununua dawa za viuajisumu na kumeza bila maelekezo yoyote kutoka kwa mtaalam wa afya jambo linalochangia usugu wa vimelea vya nagonjwa, " alisisitiza Dk Fimbo. 

Dk Fimbo alisema hata wagonjwa hao wanapotumia dawa hizo wengi hawafuati dose kamili na badala yake kuishia njiani. 

" Mtu akishaanza kupata nafuu tu anakatiza dose jambo ambalo halishauriwi kitatibu, " aliongeza Dk Fimbo.


 

0/Post a Comment/Comments