HAKUNA WA KUSHINDANA NA DKT SAMIA UCHAGUZI 2025

*******

    Mjumbe wa halmashauri kuu ccm taifa (NEC) *ndugu Ndele Mwaselela* amewaambia wananchi wa mkoa wa kagera kuwa kazi nzuri za *Dkt Samia Suluhu Hassan* kwa miaka minne katika sekta zote zimefanya wananchi wa nchi nzima Tanzania kumpenda na kumwamini Dkt Samia Suluhu, kila mahala tunapopita wana imani kubwa na Dkt Samia Suluhu Hassan. 

     Ndugu Mwaselela, amewaomba watanzania wote kutoka bara na visiwani kwenda kumchangua *Dkt Samia Suluhu Hassan* kwa kura nyingi na wagombea wa udiwani kupitia ccm na wabunge kupitia CCM.

  "Twendeni tukaionyeshe Dunia kuwa tuna Rais bingwa wa kuleta maendeleo ya wananchi wote ,tuwaambie tuna *Dkt Samia Suluhu Hassan* ambae ni bingwa wa Diplomasia na bingwa wa Demokrasia ya kweli".

kwa namna ya alivyomchapa kazi hatuna mtu wa kumshinda mgombea wetu *Dkt Samia Suluhu Hassan* na mgombea mweza *Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi.*

 Wito huo ameutoa, akiwa katika ziara ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa *Ndugu Stephen Wasira* Katika Mkoa wa Kagera.

*#Kazi na Utu, Tunasonga Mbele*
 

0/Post a Comment/Comments