****
Katika muendelezo wa kusheherekea miaka 30 ya kuleta mabadiliko katika jamii, Benki ya CRDB imekabidhi madarasa mawili na vyoo sita katika kwa Shule ya Msingi Misufini iliyopo kata Magoroto Wilaya ya Muheza.
Madarasa hayo yamekabidhiwa kwa niaba ya Benki ya CRDB na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Miranda Mpogolo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza, Mhe. Hamisi Mwinjuma.
Bi. Miranda amesema Benki ya CRDB inajivunia kuwa mdau wa maendeleo na kushirikiana na Serikali katika kuwezesha jamii kupitia sera yake ya uwekezaji katika jamii inayoitaka Benki kutoa asilimia moja ya faida yake kuwekeza katika jamii.
Kwa upande wake, Mhe. Hamisi Mwinjuma ameishukuru Benki ya CRDB kwa uwekezaji huo ambao unakwenda kuwapa ahueni wanafunzi wa kata hiyo ambao walikua wanatembea zaidi ya kilomita tano hadi sita kwa siku kufika shuleni huku wakishindwa kufika shuleni kabisa kipindi cha masika.
Post a Comment