TANZIA:
Mwanasiasa mkongwe na Waziri wa zamani wa Elimu Thabita Siwale amefariki dunia jana usiku akiwa na umri wa miaka 86.
Kwa mujibu wa ukurasa wa mchambuzi wa siasa za kimataifa Maggid Mjengwa kwenye mtandao wa Facebook , msiba uko nyumbani kwake Mikocheni.
Bi Tabitha Ijumba Mwambenja, mke wa Marehemu Mzee Siwale alizaliwa Mkoani Mbeya, mwaka 1939 kwenye Ukoo wa Mwambenja na damu yake inasemekana kuwa na mahusiano ya karibu na Ukoo wa Chifu Mwakatumbula.
Kutokana na kuolewa na kuwa mke wa Mzee Siwale amekuja kujulikana sana kwa jina la "Mama Siwale", Alianza kupenda siasa akiwa mtoto kabla ya Uhuru wa Tanganyika, akijipenyeza katika mikutano ya TANU kusikia yanayozungumzwa, ingawa baba yake alikuwa akimkataza kujihusisha na siasa na kumtaka asome kwanza, lakini yeye hakuacha siasa.

Post a Comment