MAMBO 12 MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA TMDA


 *****

Na Tausi Mbowe

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imetekeleza mambo 12 katika Awamu ya Sita ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madarakani ikiwa ni pamoja na kusajiliwa viwanda 18 vya dawa, 140 vya vifaa tiba na Vitendanishi hivyo kuchangia katika uwekezaji. 

Vileviile TMDA katika kipindi cha miaka minne imesajili zaidi ya bidhaa 8303 za dawa na 3,019 za Vifaa Tiba na Vitendanishi baada ya kujiriddhisha na ubora na ufanisi wake. 

Lingine ni kuongeza bajeti kulilowezesha utoaji wa huduma kwa ufanisi na kutoa gawio la Sh23. 3 bilioni kwa Serikali, uwekezaji wa Sh15 bilioni katika ununuzi wa vifaa vya kisasa vya maabara ili kuwezesha kufanya maamuzi ya kisayansi.  

Pia matumizi ya mifumo ya kielotrinic katika huduma za utoaji vibali jambo lililowesha kutolewa kwa saa 24,kuendelea kushikiria cheti cha Ithibati na Ithibati ya Maabara kwa kiwango cha ISO katika utoaji wa huduma bora. 

Imewezesha asilimia 98 ya bidhaa kukidhi ubora na ufanisi hivyo kuhakikusha usalama wa bidhaa za dawa na vifaa tiba katika soko, kuogeza maabara hamishika mara dufu kutoka 19 hadi kufikia 28 ili kuimarisha zoezi la uchunguzi wa sampuli. 

Imekamilisha ujenzi wa miundombinu ya tanuri la kuteketeza zisizofaa lililopoa eneo la Nala jijino Dodoma ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia katika soko ni zile tu zenye ubora, ufanisi na usalama na kuongeza wafanyakazi kutoka 278 hadi kufikia 421 hivyo kuongeza fursa ya ajira nchini. 

Lingine ni ongezeko la vituo vya ufuatiliaji wa mahudhu ya dawa pamoja na upanuzi wa ofisi kwa kuongeza sakafu tatu kwenye jengo la ofisi ya Makao Makuu Dodoma.

0/Post a Comment/Comments