MBETO AMSHANGAA OMO KUSHINDWA KUINGIA ANGOLA


 ******

Na Mwandishi  Maalum,  Zanzibar 

Idara ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo CCM Zanz. 

Kamati  maalum ya NEC  Zanzibar imemshangaa Mwenyekiti   wa ACT  Wazalendo, Othman Masoud Othman,  kutojua  itifaki za safari za viongozi na kujikuta akikwama kuingia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa  wa Angola. 

Pia idara  hiyo  imesema  endapo Othman  hajui hata  utaratibu  wa safari za nje , kushindwa kuujulisha ubalozi ,ni wazi  hana uwezo wa kuwa Rais  wa Zanzibar .

Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Nec na  Katibu  wa Kamati Maalum ya Nec zanzibar ,Khmis Mbeto  Khamis , aliyesema kiongozi  huyo amelitia aibu  Taifa akiwa ughaibuni 

Mbeto alisema kutokana na wadhifa  wake wa  Makamo wa Kwanza wa Rais SMZ, alitakiwa kuaga kazini , kutoa taarifa Wizara ya Mambo ya Nje na kujulisha Ubolozi wa Tanzania  Angola .

Aliongeza kusema taratibu  hizo humfanya kiongozi wa Serikali kuanza  kuandaliwa taribu za kiitifaki ,kiusalama na za kidiplomasia .

"Mwenyekiti  wa ACT  ametuabisha kwa kukiuka taratibu na  itifaki za  kidiplomrasia .Makamo wa kwanza wa Rais  hawezi kuingia nchi yoyote  kienyeji.Lazima  taratibu zifuatwe na  maafisa ubalozi wazisimamie" Alisema  Mbeto. 

Aidha   alisema hata kama Mwenyekiti    wa ACT  alikuwa na mpango  wa  kukutana na viongozi wa UNITA ili kujifunza sera ,mbinu na mikakati ya  kimapambano, alipaswa kufuata taratibu.

"Kabla ya kwenda  Angola OMO alishatoa msimamo wa  ACT wa  kuweka kando siasa za maridhiano na kuanzisha mapambano. UNITA cha Angola  na RENAMO  cha Msumbiji ,vina uzoefu mkubwa wa siasa za mapambano" Alieleza  Mbeto .

Viongozi  waliowahi kuviongoza UNITA cha Angala  na Renamo  cha Msumbiji ni Jonas Savimbi na Alfonso Dlakama ambao sasa wote ni marehemu .

Katika maelezo  ya Katibu  huyo Mwenezi, alisema dunia nzima inajua Jamhuri  ya Muungano  wa Tanzania ni Muungano wa Tanganyika  na Zanzibar, hivyo kiongozi  kutoka upande  wowote , hupokewa kwa uzito  uleule.

'CCM itaendelea kuamini na kufanya siasa za kimaridhiano. Hakitajiingiza katika  siasa za kimapambano. Wakati wa mapambano umepita. Afrika  nzima sasa  iko huru. Kutangaza za mapambano ni kutamani sera za kiharamia" Alisema Mbeto 

Hata hivyo alivitaka vyama vya upinzani vya Tanzania, kutambua kuwa mchango  wa  Tanzania katika nchi za Kusini  mwa Afrika unaheshimiwa lakini pia  CCM na vyama vya vilivyokuwa vua ukombozi ni ndugu  wa damu.

0/Post a Comment/Comments