MBETO : SI LISSU WALA HECHE KWA DKT SAMIA 2025


****

Katibu Kamati Maalum NEC, Zanzibar, Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema kutokana na mafanikio ya serikali inayoongozwa na Rais  Dkt.  Samia  Suluhu Hassan ni ngumu kwa wananchi  kusikiliza propaganda za viongozi wa Chadema kuwa hakuna maendeleo yaliyopatikana.

Mbeto alisema chini ya Dkt Samia maendeleo yamepatikana kila sekta.

"Wakati tunapata uhuru 1961 asilimia 70 ya watanzania walikuwa hawajui kusoma, wala kuandika, leo asilimia 83 wanajua yote mawili" alisema.

Alibainisha Mbeto kuwa leo kila kata ina shule ya sekondari. 

Sera ya elimu na mafunzo ya 2014, toleo la 2023 inabainisha kuwapa uwezo vijana katika elimu na stadi kuukabili ushindani kikanda na kiulimwengu.

"Tuna vyuo vikuu 35 na 15 vishiriki, utasemaje hakuna  maendeleo" alisema.

 Mbeto alibainisha kuwa ulimwengu pia unatambua jiitihada zake ktk masuala ya kijamii na usalama.

Alisema Tuzo ya Kimataifa ya Goalkeeper  Award ya Gates Foundition na mkutano wa SADC na EAC kuhusu DR  Kongo vimempa heshima  yeye binafsi na Taifa kwa ujumla.

"Kafanya mengi sana ambayo  ni historia ktk nchi na ulimwengu kwa ujumla ikiwemo mikataba yenye tija kwa Taifa" alisema Mbeto.

Alibainisha  uungwana kuridhia takwa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) la kuwepo kliniki za kisheria ambazo hadi sasa zinazunguka nchi nzima.

"Maendeleo ni hatua na wananchi wanayo yaona wanayafurahi" alisema.

Mbeto anabainisha kuwa upinzani utasubiri sana kwani mengi yanafanyika na kubwa zaidi kuufungua mkoa wa viwanda Tanga kwa kuweka mikakati kufufuliwa viwanda vilivyokuwepo, upanuzi na ujenzi wa Bandari ya Tanga na umeme wa uhakika wenye msongo mkubwa kutoka Ethiopia.

"Lissu na Heche hawajielewi hata Chadema yenyewe ipo vipande, vipande " alisema.

Mwisho

0/Post a Comment/Comments