MBUNGE LUSINDE ATAJA UIMARA WA RAIS DK.SAMIA MIAKA MINNE MADARAKANI

****

MBUNGE wa Jimbo la Mvumi, mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa Mapinduzi makubwa ya mafanikio katika miaka yake minne ya uongozi madarakani.

Mbunge Lusinde ameyasema hayo kupitia mahojiano maalum ya miaka minne ya Rais Dk. Samia madarakani.

"Rais Dk.Samia amefanya kazi kubwa yenye mapinduzi makubwa ya kiuchumi. Wakati akiingia madarakani hakuwa na maneno mengi, lakini alijikita katika vitendo vya kutekeleza miradi yote ya maendeleo iliyoachwa na mtangulizi wake, hakuna mradi wowote ulioachwa yote mikubwa iliyogharimu matrilioni ya fedha ameyatekeleza," alieleza.

Alieleza kuwa, katika miaka minne ya Rais Dk.Samia amefanya mambo makubwa nchini, ikiwemo miradi ya kimkakati kama Bwawa la umemae la Julius Nyerere, Daraj la Kigongo Busisi, Daraja la Pangani, reli ya kisasa ya SGR, ununuzi wa Ndege, tuna kila sababu ya kumuunga mkono.

Alisema kwa kazi hizo, tunatakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais Dk.Samia na kumchagua tena katika miaka mingine mitano hadi 2030, aendelee kuchochea maendeleo ya Taifa.

JIMBONI MVUMI 

Akielezea utekelezaji Ilani Jimbo la Mvumi, Mbunge Lusinde alieleza kuwa, katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dk.Samia miradi mingi imetekelezwa hivyo kuondoa changamoto mbalimbali za wananchi katika kupata huduma.

Alisema wananchi wa Mvumi wamepata shule mpya za elimu ya awali, msingi na sekondari, miradi ya maji imetekelezwa, nishati ya umeme imeunganishwa kwa wananchi.

"Tumepata miradi ya maji iliyogharimu sh. bilioni moja kasoro kidogo, katika kata ya Mvumi mission na Kata ya Angali, kuanza kutekelezwa kwa Barabara iliyopo Tarafa ya Mvumi ambapo fedha zimetolewa na serikali na hivi karibuni Wizara ya Fedha ilisaini mikataba ya kuanza ujenzi huo, jambo ambalo litaondoa kero kubwa kwa wannachi," alisema.

Alisema wanamshukuru sana Rais Dk.Samia kwa kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa barabara hiyo muhimu itakayo waunganisha Wananchi wa Mvumi na Dodoma Mjini, hivyo kufungua uchumi wa wananchi hao kwani watapata wepessi wa kupeleka bidhaa zao za nyanya na mapapai masoko ya mjini.

Alisema Mvumi wanajivunia uongozi wa Rais Dk.Samia katika miaka yake minne madarakani na wannamshukuru sana, hawana cha kumlipa zaidi ya kumpa kura nyingi za ushindi.

Aliwataka Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Dk.Samia kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kutoa fedha nyingi za maendeleo katika mikoa na majimbo mbalimbali, hivyo wamuunge mkono na kumchagua kwa kura nyingi katika Uchaguzi wa mwaka huu.


 

0/Post a Comment/Comments