*****
Bodi ya Ligi kupitia Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu imeahirisha mchezo wa leo wa Yanga SC dhidi ya Simba SC ili kutoa nafasi ya kupata taarifa zaidi zitakazosaidia kufanya maamuzi ya haki, baada ya Simba kulalamika kuzuiliwa kuingia kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa kwa ajili ya mazoezi ya mwisho.
Bodi imesema itatoa taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo na kutangaza tarehe ya mchezo huo mapema iwezekanavyo.
Post a Comment